Kwa lugha ya kitalaamu ugonjwa huu hujulikana kama Peri-anal fistula au (Fistula in ano). Ni tatizo la kuwapo kwa tundu au matundu karibu na njia ya haja kubwa.
Tundu hilo huwa na mfereji unaojitokeza katika njia ya haja kubwa kwa ndani na hupitisha choo kikubwa bila ya mgonjwa kujitambua au kufahamu. Tatizo hili huwakumba watu wanawake hata wanaume.
Dalili
Dalili za ugonjwa huu ni maumivu, kutokwa haja kubwa laini bila mgonjwa kujitambua, hivyo kuchafua nguo.
Hali hii humsababishia mgonjwa msongo wa mawazo, kutokujiamini na adha katika jamii kutokana na kutoa majimaji hayo ya choo ambayo huwa na harufu mbaya.
Dalili nyingine ni kuota kinyama sehemu za siri ambacho ndiyo mdomo wa nje wa fistula.
Ugonjwa huu wa fistula katika makalio husababishwa zaidi na jipu katika maeneo hayo. Karibu asilimia 30 ya watu wanaopata jipu katika makalio ambalo halikutibiwa ipasavyo huishia kupata adha hii kubwa ya fistula ya njia ya haja kubwa.
TB(tuberculosis), magonjwa ya zinaa, michubuko au vidonda vingi vya muda mrefu katika utumbo mpana (ulcerative colitis, crohon’s ), pia huchangia kutokea kwa fistula ya njia ya haja kubwa, bila kusahau saratani ya njia ya haja kubwa pia.
Ni vyema litokeapo tatizo hili mgonjwa aende hospitalini kupata matibabu kwa kuwa tatizo hili lina tiba. Vipimo vinavyoweza kufanyika kuchunguza ukubwa wa tatizo na kupanga tiba au upasuaji ni pamoja na altrasaundi kupitia njia kubwa au MRI. Kipimo hiki ni kizuri, lakini ni cha gharama kubwa na hakipatikani kwa urahisi. Lakini huweza kuonyesha ukubwa wa tatizo, hasa matundu yanapokuwa mengi.
Kipimo kingine ambacho hakitumiki sana siku hizi ni Fistulography (kuweka dawa maalumu na kisha kupiga X-ray)
Matibabu ya ugonjwa huu ni upasuaji.
Fistula iliyo kwa chini ni rahisi kwani tundu lake hukatwa na kuwekwa wazi. Fistula iliyokwenda juu zaidi uhitaji kuwekewa uzi maalumu na matibabu yake huchukua miezi kadhaa hadi kupona. Gundi maalumu hutumika pia kuziba fistula. Ni muhimu kutibu tatizo lililoleta ugonjwa huo mfano Tb na magonjwa ya zinaa kama ilivyo ainishwa hapo juu.
Unjwa wa fistula na matibabu yeke
Title: Unjwa wa fistula na matibabu yeke
Author: Mpanda israel
Rating 5 of 5 Des:
Author: Mpanda israel
Rating 5 of 5 Des:
Kwa lugha ya kitalaamu ugonjwa huu hujulikana kama Peri-anal fistula au (Fistula in ano). Ni tatizo la kuwapo kwa tundu au matundu karibu ...
Post a Comment