Washington, Marekani. Maofisa wa idara ya uhamiaji nchini Marekani wameripotiwa kuanza kuchunguza kurasa za kijamii na hasa za mtandao wa Facebook kwa wasafiri ili kubaini misimamo yao ya kisiasa.
Hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Rais Donald Trump, ambaye amesaini hati kadhaa zinazobainisha msimamo wa Serikali yake.
Kwa mujibu wa gazeti la Independent, Wakili wa masuala ya Uhamiaji, Mana Yegani aliye mjini Houston, alisema wasafiri kadhaa wenye kadi ya ‘Green Card’ ambayo inawapa ruhusa ya kuishi na kufanya kazi Marekani, wamesimamishwa na maofisa wa uhamiaji katika viwanja vya ndege na kuhojiwa kwa saa kadhaa.
Mtaalamu huyo wa sheria alisema maofisa wa usalama katika mipaka ya Marekani wanachunguza kurasa za Facebook za wasafiri kubaini mitazamo yao ya kisiasa kabla ya kuwaruhusu kuingia nchini humo.
Hatua hiyo ya kupiga marufuku raia wa kigeni kutoka mataifa saba kuingia nchini Marekani imesababisha maandamano makubwa ya wananchi.
Wahamiaji wachunguzwa Face book
Title: Wahamiaji wachunguzwa Face book
Author: Mpanda israel
Rating 5 of 5 Des:
Author: Mpanda israel
Rating 5 of 5 Des:
Washington, Marekani. Maofisa wa idara ya uhamiaji nchini Marekani wameripotiwa kuanza kuchunguza kurasa za kijamii na hasa za mtandao wa ...
Post a Comment