PAA za madarasa sita ya Shule ya Sekondari Kisumwa iliyopo katika Tarafa ya Suba mkoani Mara pamoja na nyumba za walimu na choo, zimeezuliwa na mvua kubwa iliyoambatana na upepo.
Mvua hiyo iliyonyesha mwishoni mwa wiki, pia imeharibu nyumba na mazao ya wakazi wa vijiji vya Kisumwa na Mara Sibora mkoani Mara.
Akizungumza na Nipashe mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, Charles Chacha, alithibitisha kuwapo kwa tukio hilo.
Chacha alisema mvua hiyo ilinyesha wilayani Rorya ikiwa ni baada ya zaidi za mwezi mzima ikikumbwa na ukame.
Alisema mvua hiyo iliyokuwa imeambatana na upepo mkali, iliezua paa za madarasa sita, nyumba ya mwalimu na choo katika Shule ya Sekondari Kisumwa.
Kadhalika, Chacha alisema mvua hiyo pia iliharibu mazao na baadhi ya nyumba za wakazi wa vijiji vya Kisumwa na Mara Sibora.
Alisema Kamati ya Maafa chini ya Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Saimon Chacha, itafanya tathmini ya mali iliyoharibika katika shule hiyo na kwa wakazi wa vijiji hivyo.
Aidha, Mkurugenzi huyo amewahimiza wananchi wa Wilaya ya Rorya kuzitumia mvua zinazoendelea kunyesha kupanda mazao yanayokomaa kwa muda mfupi na yanayovumilia ukame.
Mvua yaezua paa za madarasa sita na choo
Title: Mvua yaezua paa za madarasa sita na choo
Author: Mpanda israel
Rating 5 of 5 Des:
Author: Mpanda israel
Rating 5 of 5 Des:
PAA za madarasa sita ya Shule ya Sekondari Kisumwa iliyopo katika Tarafa ya Suba mkoani Mara pamoja na nyumba za walimu na choo, zimeezuli...
Post a Comment