Wachawi wana uwezo wa kumtia mtu nuksi na mikosi mbalimbali.
Nuksi na mikosi hiyo inaweza kuja katika sura ya magonjwa na maradhi sugu yasiyopona kama vile kisukari, ukimwi, ugumba, mimba kuchoropoka, kifafa nakadhalika.
Kufukuzwa kazi, matatizo katika ndoa, ajali, umasikini, vifo na misiba mfululizo, kuchukiwa na watu nakadhalika.
Zipo njia mbalimbali wanazo tumia wachawi katika kuwatia watu nuksi na mikosi, Katika makala ya leo, nitaelezea njia moja wapo kama ifuatavyo:
Katika njia hii, wachawi wakitaka kumtia mtu mikosi, hufanya mambo yafuatayo :
i. Wanachukua hela ambayo haitumiki
ii. Wanachukua mavi ya mbwa mweusi ambayo ameyanya usiku wa manane
iii.Wanachukua mkaa ulio kwisha tumika, ambao umetumika mahali ambapo watu hawalali kama vile kilioni au kwenye baa na migawaha inayo kesha lakini mara nyingi, huchukua mkaa wa kilioni.
iv.Wanachukua mavi ya ndege anaitwa Mumbi. Huyu ndege aitwae Mumbi anapatikana porini. Anafanana sana na bata na ana puyanga la rangi nyekundu.
v. Wanachukua shahidi la kaburini pamoja na ndumba zingine za kichawi
vi. Wanachukua kitu chochote cha mtu aliye kusudiwa kutiwa mikosi kama vile jina lake, picha yake, mchanga alipokanyagia, mate, kucha, au chochote kile.
Baada ya hapo, mchawi huyo atakwenda kaburini usiku wa manane na kuvizika vitu vyote nilivyo vieleza hapo juu, huku akisema maneno ya kichawi. Basi mtu aliye kusudiwa na uchawi huu, kama hana kinga, ata andamwa na mikosi mikubwa na mizito katika maisha yake yote.
JINSI YA KUJIKINGA DHIDI YA UCHAWI HUU
Kujikinga na uchawi huu inabidi ufanyiwe zindiko ama upate kinga maalumu ya kuficha kivuli chako. Hii itawafanya wachawi washindwe kukuona katika rada zao za kichawi, na wachawi huwa hawawezi kumloga mtu ambae haonekani katika rada zao, kwa sababu wanawakuwa hawajui nguvu zake ziko wapi wala silaha zao haziwezi kumshambulia mtu ambae haonekani kwenye rada zao.
Ukiwa na kinga hii, hakuna uchawi wa aina yoyote ile unao weza kufanyika juu yako, iwe ni uchawi wa kukusababishia madhara, au uchawi wa mahaba kukufunga kimapenzi.
JINSI YA KUFICHA KIVULI CHAKO KISIONEKANE NA WACHAWI
Kuficha kivuli chako kisonekane na wachawi, fanya kama ifuatavyo
i. Chukua nywele za saluni
ii. Chukua mzizi wa mti ulio katisha njia
iii. Chukua tawi la mti unaitwa Ututukanga. Huu mti wa Ututukanga unapatikana porini na baharini na huwa linaonekana shina lake na matawi yake tu, lakini mzizi wake huwa hauonekani.
iv. Unachukua mti unaitwa Msonihya
v. Unasaga pamoja na mti unaitwa mwavi.
vi. Baada ya hapo unachukua kuku mweusi, unamfunga kwenye kitambaa cheusi bila kumchinja, unachukua chungu cheusi, unamuunguza mpaka anakuwa mkaa, halafu unamsaga pamoja na miti iliyo tajwa hapo juu, unachanganya na mafuta ya simba.
vii. Unachukua buja ama dulya la ugali wa kilioni
viii.Unachukua kamba ya kitanda alicho lalia maiti, au kama maiti ipo kwenye nyumba ya nyasi, unachomoa nyasi wakati maiti imo ndani.
ix. Unachimba mzizi wa mti unaitwa mputika bila kivuli chako kugusa mti..
x. Unaunguza vyote kwa pamoja ukiwa na kaniki nyeusi bila kuvaa nguo yoyote usiku wa manane
xi. Unaipika njia panda pamoja na mafuta ya usiku.
Baada ya hapo, mtu atachanjiwa au kujichanja mwenyewe na kuoga au kuogeshwa dawa hiyo.
Basi wachawi watakuwa wakijaribu kutaka kukutupia uchawi, wanakuwa hawakauoni kwenye rada zao za kichawi.
IMESIMULIWA NA DOKTA. MUNGWA KABILI….0744 000 473.
Post a Comment