Mpanda israel Mpanda israel Author
Title: Mjadala wa kesi ya Lufunga ndani ya Sports Extra
Author: Mpanda israel
Rating 5 of 5 Des:
Maamuzi ambayo yametolewa na Kamati ya saa 72 ya TFF kuhusu rufaa ya Polisi Dar dhidi ya mchezaji wa Simba Novalty Lufunga imekuwa ni issue...

Maamuzi ambayo yametolewa na Kamati ya saa 72 ya TFF kuhusu rufaa ya Polisi Dar dhidi ya mchezaji wa Simba Novalty Lufunga imekuwa ni issue ambayo ina-trend sana kwenye mitandao ya kijamii pamoja na vyombo vya habari hapa nchini.
January 26, 2017 kwenye kipindi cha Sports Extra cha Clouds FM kulikuwa na mjadala mkali kuhusu uamuzi uliotolewa na kamati ya saa 72 kwa kuitupilia mbali rufaa ya Polisi Dar kwa madai kwamba kuna baadhi ya mambo hayakuzingatiwa katika kukata rufaa hiyo.
Mjadala huo uliibua mambo kadhaa kwa kuzingatia kanuni na taratibu za shindano husika na kuibua hoja kadhaa ambazo kama TFF watazijibu basi moja kwa moja utagundua Polisi Dar wamepokwa haki yao.
Picha lilipoanzia
Lufunga alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kuoneshwa kadi ya pili ya njano kwenye mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Coastal Union kwenye uwanja wa taifa ambapo Simba walipoteza mechi hiyo kwa kufungwa goli 1-0 msimu uliopita (2015/2016).
Kwa mujibu wa kanuni za mashindano ya kombe la FA, Lufunga alitakiwa kukosa mechi moja ya michuano hiyo ili kutumikia adhabu yake ya msimu uliopita lakini cha kushangaza mchezaji huyo alipagwa kama mchezaji wa akiba kwenye mechi dhidi ya Polisi Dar ambayo Simba ilishinda kwa magoli 2-0. (ambao ni mchezo wa kwanza kwa Simba tangu ilipocheza mara ya mwisho na Coastal Union).
Kanuni ya 22 kombe la shirikisho
Udhibiti wa wachezaji
Mchezaji yeyote atakayefanya jambo kinyume cha kanuni za nidhamu ataadhibiwa kwa kufuata kanuni za ligi kuu.
Kanuni za ligi kuu kuhusu udhibiti wa wachezaji
Sura ya 11 udhibiti wa wachezaji
Mchezaji atakaetolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kadi mbili za njano (second yellow card) katika mchezo wa ligi hata ruhusiwa kucheza mchezo mmoja unaofata wa timu yake.
Kanuni za kombe la FA kuhusu mchezaji atakaetolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kuoneshwa kadi mbili za njano, kanuni inaelekeza mchezaji huyo hatoruhusiwa kucheza mchezo mmoja unaofuata wa timu yake.
Kukata rufaa au kutoka rufaa
Kama Polisi Dar walikata rufaa basi walitekeleza jukumu lao la kikanuni, lakini kama hawakukata bado wana nafasi nyingine ambayo haiwanyimi wao fursa au haki yao kwa sababu tu hawakukata rufaa na kupeleka Tsh. 300,000 ndani ya saa 72.
Ukirudi kwenye kanuni za Kombe la FA Sura ya sita kanuni ya 17 ya malalamiko inajieleza wazi, kanuni ya 17 kipengele cha tatu kinasema; ‘TFF inaweza kutolea maamuzi au kupeleka jambo lolote linalohusiana na shindano hili la kombe la shirikisho la Azam Sports HD kwenye chombo husika kwa kujadiliwa bila kujali kulalamikiwa au la.’
Wao kama shirikisho, kazi yao ni kusimamia kanuni ambazo walizitunga wao wenyewe, mchezaji hatakiwi kucheza lakini amecheza sio lazima Polisi Dar ijue mchezaji fulani alikuwa na kosa hakupaswa kucheza, sio jukumu lao ni jukumu la shirikisho kusimamia kanuni zao.
Haiwezekani TFF au hiyo kamati ya saa 72 iseme Polisi Dar haikukata rufaa au kuwasilisha pesa ndani ya muda. Kwa hiyo kama Polisi Dar hawakukata rufaa na kuwasilisha pesa ndani ya muda basi kanuni zivunjwe.
Kikubwa hapa ni kwamba, Lufunga alioneshwa kadi au hakuoneshwa kadi? Kama alioneshwa kadi kanuni za mashindano zinasemaje?
Inasemekana kadi za njano na nyekundu zinakoma mwisho wa msimu wa mashindano husika, lakini hii kanuni imeandikwa wapi mbona haionekani kwenye kanuni za mashindano?
Kama ni mfatiliaji mzuri wa mambo ya soka naamini unakumbuka kilichowakuta Real Madrid kwenye kombe la Mfalme msimu uliopita, Madrid walichezesha mchezaji ambaye hakupaswa kucheza lakini haki ilitendeka kwa Madrid kuondoshwa kwenye mashindano kwa sababu watu hawakuangalia ukubwa wa Madrid badala yake kanuni ndizo zilitumika.
Lakini kama kosa limetendeka basi kila mtu apate anachostahili, hili ni kosa la kikanuni tusifanye mambo kwa ajili ya kuzuia watu fulani wasiathirike. Sio dhambi kumuadhibu mtu kwa kosa la kikanuni kuliko haya yanayofanyika ya kutengenezesha mambo na kuwaaminisha watu ujinga.

27 Jan 2017

About Author

Advertisement

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top