Mpanda israel Mpanda israel Author
Title: Tazama kitita alichokikataa Tevez
Author: Mpanda israel
Rating 5 of 5 Des:
Baada ya Tevez kusajiliwa kwenda Shanghai Shenhua mshahara wake ulitajwa kuvunja rekodi ya dunia.Taarifa zinasema Tevez atapewa £615,...

Baada ya Tevez kusajiliwa kwenda Shanghai Shenhua mshahara wake ulitajwa kuvunja rekodi ya dunia.Taarifa zinasema Tevez atapewa £615,000 kwa wiki akiwa na timu yake hiyo mpya.Mshahara huo unamfanya Tevez kuwa mwanasoka anayelipwa zaidi duniani kwa sasa.

Sasa Carlos Tevez amekanusha kuhusu hela hiyo anayolipwa.Kwa mara ya kwanza Tevez akifanya mahojiano na waandishi wa habari China Teves alisema “Baada ya mechi yangu ya mwisho nikiwa na Boca Juniours sikuwahi kuongea na vyombo vya habari kuhusu mshahara wangu”.

Masuala ya mshahara ni kati yangu na mwajiri na sio na mtu mwingine,sii vyema kuwaambia watu kuhusu kipato chako,ni suala la heshima kwa wachezaji wenzangu,sina mshahara mkubwa na siwezi kusema ni kiasi gani” aliongeza Tevez ambaye pia aliwashukuru wanafamilia wake kwa ushirikiano wao na kuishukuru timu yake ya zamani ya Boca Juniours.

Carlos Teves amehamia China rasmi,katika kuhama huko Tevez amebeba watu 19 wa familia yake na kuhamia nao nchini China.Alisema familia yake ndio inamfanya acheze mpira vizuri na hivyo kukaa karibu na familia yake kutampa kiwango bora uwanjani.Haijawekwa wazi na yeye binafsi ni kiasi gani analipwa akiwa Shenhua lakini ameweka wazi kwamba sio kiasi hicho kinachotajwa na vyombo vya habari

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top