TULIKOSEA SANA KUMDHIHAKI KIKWETE
Salamu kwako ewe Rais wa watu, uliyekataa kuwa mtawala na ulipenda kuwa kiongozi. Kiongozi uliyekubali kukosolewa ukampokea Ikulu kila Mtanzania mwenye shauku ya kukuona. Ulizungumza kwa tabasam na kukaa kimya hata pale ulipodhihakiwa na kudhalilishwa. Huruma na Upole wako viliificha kabisa hasira yako.
Sio tu kwanza uliwatumia Wapinzani kwa kuwapa hoja na evidence ili wawakosoe Watendaji wako kwa hoja. Uliimarisha Upinzani kwa siri na dhahiri, kwani uchaguzi wa 2010 ulimpigia kampeni kwa wazi ndugu Zitto Kabwe na ukamwacha mgombea wa chama chako na ilhali wewe ni mwenyekiti wa chama.
Chama chako kilikataa wazi kuwa Hakitaki katiba mpya wewe ulijitokeza wazi na kusema Kuna Haja ya Tanzania kuwa na katiba mpya nasio marekebisho. You're such an amazing president Dr JK
Ulituonea huruma Watanzania ukaacha kutunyang'anya kidogo tunachomiliki kulipia kodi badala yake ulikwenda nje kutafuta misaada isiyokuwa na masharti. Leo tuna kamuana kweli kweli kuchangia mapato.
Katika Uongozi wako vyuo vingi vimeanzishwa, hakuna mtendaji aliyekuwa na nidhamu ya woga, watu wamejenga nyumba wakamiliki magari mengi kiasi ambacho hata omba omba walifurahia Uongozi wako.
Licha ya wakosoaji wako kuuficha Uzuri wako, lakini wengi tuliuona. Leo hii hakuna yeyote ktk Wakosoaji wale anayekutaja kwa Ubaya kuliko kiongozi wa zama hii.
WE MISS YOU JK WHERE ARE YOU?
© kwa msaada wa Adnan Mahmoud
Post a Comment