Mpanda israel Mpanda israel Author
Title: Mwanjale atacheza Simba vs Yanga? Daktari katoa majibu yake…
Author: Mpanda israel
Rating 5 of 5 Des:
alishindwa kumaliza dakika 90 baada ya kupata majeraha kwenye mguu wake wa kushoto wakati Simba ikicheza dhidi ya Tanzania Prisons kwenye uw...
alishindwa kumaliza dakika 90 baada ya kupata majeraha kwenye mguu wake wa kushoto wakati Simba ikicheza dhidi ya Tanzania Prisons kwenye uwanja wa taifa.

Mwanjale aligongana na mchezaji wa Prisons wakati wakiwa kwenye harakati za kuwania mpira, akatibiwa na kuendelea kucheza lakini baadae alishindwa kuendelea na mchezo na kupelekea kutolewa nje kwa msaada wa machela.

Bada ya mechi kumalizika, shaffihdauda.co.tz ilimtafuta daktari wa Simba Yassin Gembe ili azungumzie hali ya Mwanjale na ukubwa wa jeraha alililolipata kipindi cha pili cha mchezo huo.
“Si majeraha makubwa ni ya kawaida tu kwa namna nilivyofanya uchunguzi wa haraka, hata kaa nje kwa muda mrefu. Tutamfanyia vipimo zaidi ili kujua ukubwa wa tatizo”, – Yassin Gembe.

Gembe amewatoa hofu mashabiki wa Simba kwa kusema watahakikisha beki huyo wa kutumainiwa anarejea uwanjani mapema iwezekanavyo kuendelea na majukumu yake.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top